Monday, November 30, 2009

Mrema atangaza kumvaa Kimaro Vunjo

BAADA ya kushindwa kufua dafu mara tatu katika mbio za urais, hatimaye mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema amerejea kwenye kinyang'anyiro cha ubunge baada ya kutangaza kuwa atapambana na Aloyce Kimaro kuwania jimbo la Vunjo.

Mrema, ambaye amewahi kugombea urais akiwa na NCCR Mageuzi na baadaye TLP, alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20 kabla ya kutofautiana na serikali na baadaye kujiunga na upinzani katika miaka ya tisini.

Wakati hali ikionekana kumuendea kombo Kimaro kwenye jimbo hilo, Mrema anaonekana kutaka kutumia mwanya huo kurudi Vunjo ambako TLP ina nguvu kubwa.

Mwenyekiti huyo wa TLP aliliambia gazeti hili jana kuwa baada ya kumtikisa Kimaro katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu ambao chama chake kimeshinda katika vijiji 20 na vitongoji 48 dhidi ya vijiji 47 vya CCM, sasa anajipanga kwenda jimboni humo kugombea ubunge mwakani.

"Baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, sasa namtangazia rasmi Kimaro kwamba mwakani naenda Vunjo kulichukua jimbo langu. Kimaro ameshindwa kuwasaidia wananchi ndio maana wamemzomea," alisema Mrema alipoongea na Mwananchi jana.
Mrema, ambaye alikuwa waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya awamu ya pili,

No comments:

Post a Comment