Monday, November 30, 2009

KAMPUNI YA KINGUNGE YAJITETE JUU YA TAMKO LA JIJI LA DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Kampuni ya Smart Holding ya familia ya mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru, imeibuka na kujitetea kwamba, upungufu wa mapato uliojitokeza wakati wa ukusanyaji mapato kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT), ulitokana na sababu mbalimbali, zikiwemo za kutotoza ushuru baadhi ya maeneo ndani ya kituo hicho.

Utetezi huo wa kampuni hiyo, unakuja kipindi ambacho tayari jiji limetengua kazi hiyo kwa kampuni hiyo huku ikitangaza kuongezeka mapato muda mfupi baada ya halmashauri kusimamia ukusanyaji wake.

Akizungmza na Mwananchi jijini Dares Salaam juzi, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Hassani Khan, alisema jiji wasijidangnye kwa kipato wanachokipata kwa sasa kwani ni msimu tu.

Alifafanua kwamba, kupata kipato hicho kunatokana na halmashauri kuongeza wigo wa maeneo ya kukusanya kodi.

“Sisi tulipoingia mkataba na jiji wa kukusanya mapato katika kituo hicho, walituwekea mipaka yamaeneo ya kukusanya mapato na kwingine wakikusanya wenyewe jiji,’alitoa utetezi huo.

“Sehemu kama Hotel iliyopo ndani ya kituo na baadhi ya ofisi ambazo si vizuri kuzitaja na zilikuwa na mapato makubwa kutokana na umiliki wao wa sehemu karo husika, walikusanya wenyewe jiji,”aliongeza Khan.

Khani alisema kipato hicho ni kidogo tu kwa jiji kwani , wao walikuwa wakipata Sh 67 milioni, ambazo zilikuwa zinapatikana getini kwa mwezi tofauti na sehemu nyingine ukilinganisha na ukubwa wa kituo.
Alisema hali katika kituo hicho ilibadilika baada ya jiji kubanwa juu ya mapato ya kituo, wakati wa ziara yake mwanzoni mwa mwaka huu ambapo Waziri Mkuu aliagiza kufanyika kwa uchunguzi wa hesabu za uendeshaji.
Baadaye matokeo ya ukaguzi huo uliofanywa na ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, kukiwa na taarifa ya kuwepo kwa ubadhirifu na baadaye taarifa zaidi zikibaisha kuondolewa kwa kampuni hiyo kuendesha kituo hicho.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisema katika muda wote wa miaka mitano waliokuwa wakiendesha makusanyo ya ushuru walikuwa wakipata kati ya Sh1.8milioni hadi Sh 2milioni kwa siku.
Makusanyo hayo yalikuwa ni ushuru wa magari, wasindikizaji na wapokeaji wageni ambapo halmashauri ya jiji ilikuwa ikichukua Sh 1.5milioni bila ya kukosa ambazo ni asilimia 75 na kampuni yake kupata asilima 25.
Alisema mwaka 2004 ,Wizara ya fedha iliteua kampuni binafsi ya CMK ili ifanye tathimini ya kimahesabu kujua kiasi cha mapato yanayotokana na ukusanyaji wa milango pekee yanayoweza kufikia Sh 1.8milioni.

Wakati huo huo Khan alifafanua kwamba kampuni yake haijapata barua yoyote kutoka jiji juu ya kupata kazi ya ukusanyaji mapato kwenye majengo Machinga Complex.

No comments:

Post a Comment