Wednesday, February 22, 2012

Jenipher kutoka na Dhahabu 2012

MWANAMUZIKI wa mziki wa injili nchini Jenipher
Mgend anatarajia kuachaia albamu itakayotamba kwa jina la DHAHABU yenye mkusanyiko wa baadhi ya nyimbo zangu za zamani kama vile
Nini?, Nimrudishie nini Bwana, Nitafika lini?, Mbona washangaa njiani. Ulinipa
sauti na nyinginezo ambazo zilitamba miaka ya 2001 na kurudi nyuma hadi mwaka
1995. Albamu hii tayari ipo madukani katika mfumo wa audio cd yaani ni ya
kusikiliza. Maandalizi ya video hii yanafanyika na panapo manajliwa mwezi
Agosti itakuwa imekamilika.TEKE LA MAMAFilamu hii ipo madukani na
imewashirikisha watu mbalimbali kama Bahati Bukuku, Christina Matai, Senga,
Lucy Komba na Godliver a.k.a Bibi Esta. Sio filamu ya kukosa kuangalia na uzuri
wake unaweza kuiangalia ukiwa umetulia na familia yako bila kuwa na wasiwasi wa
kuanza kuwatuma watoto dukani ili wasione picha chafu.SHEREHE ZA MIAKA 15 YA
HUDUMAPanapo majaliwa na Mungu, natarajia kufanya tamasha la kusherehekea
na kumshukuru Mungu kwa miaka 15 tangu nianze huduma ya uimbaji. Tamasha au
sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 05 Agosti, 2012 katika ukumbi wa
Landmark Hotel.Video ya album ya Dhahabu itazinduuliwa siku hiyo pia.
Maandalizi ya tamasha hili yanaendelea na litapambwa na waimbaji mbalimbali
watakaoimba live siku hiyo. Sio siku ya kukosa na wote wenye mapenzi mema
wanaombwa kujitokeza kwa wingi. Tutaendelea kuhabarishana kuhusu tukio hili
kadiri siku zinavyoendelea.ALBAM MPYAMaandalizi ya album mpya
yanaendelea moyoni lakini rasmi kabisa yataanza mara baada ya tamasha la mwezi
wa Agosti na album hii mpya inatarajiwa kuingia sokoni mwezi Aprili mwaka 2013,
tukijaliwa uzima.

No comments:

Post a Comment