Mwandishi
wetu
BAADA
ya wasanii wa muziki kuhama hama katika makundi yao walionza nayo kazi taswira
imebadilika sasa katika kundi la Mashauzi Classic kuonokewa na wasanii wanne,
ambako kila anayeamua kuchomoka, huibua kashfa nzito, hususan kumwelekea Isha
mwenyewe.
Wasanii
hao waliongoka ni Rahma Machupa, Zainab Machupa, Ashura Machupa na Hanifa
Maulid.
Wapo
walioondoka kwa kudai kuwa wamechoshwa na ubinafsi, chuki, majungu na roho
mbaya ndani ya kundi hilo, vinavyotiwa chumvi na Isha mwenyewe, huku wengine
wakisema, wivu wa Isha kwa Thabit Abdul unawaweka katika wakati mgumu.
Wiki
iliyopita nilibahatika kumtazama Isha alipokuwa
Isha
athibitishe shutuma nyingi hizi na zile anazotupiwa na baadhi ya wasanii
wanaohama Mashauzi Classic, ambako alitoa majibu yaliyojaa hekima za hali ya
juu kiasi cha kunipa msukumo wa kumtafuta ili nipate maelezo ya kina kutoka
kwake.
“Unajua,
yote yanayosemwa yanasemwa na watu kama mimi, wenye midomo na uhuru wa kuongea,
kwahiyo inakuwa vigumu kuyazuia,” ndivyo anavyoanza kueleza Isha anayetamba
sasa na kibao ‘Si Bure Una Mapungufu’, baada ya kukutana naye nyumbani kwake,
Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Isha
anasema kuwa, mengi yanayovumishwa kila uchao juu yake yanakosa makali zaidi
kutokana na yeye mwenyewe kuamua kukaa kimya bila kujibu, ambako anadai
usipiomjibu mtu tayari umemwambia anyamaze.
Anasema,
kinachomsikitisha zaidi na zaidi ni kuona kuwa, wote wanaomzushia kashfa na
shutuma hizo ni wale chipukizi ambao.
Kwa
namna hii ama ile, nguvu zake zimetumika ipasavyo kuwafikisha hapo walipo sasa.
Anazidi
kusema kuwa, kwa upande wake anaona kuwa si vema kwa wasanii wanaochipukia
katika muziki kujiingiza katika utamaduni wa kutafuta umaarufu kwa nguvu na
badala yake wajibidiishe jukwaani kupitia vipaji walivyonavyo.
Anasema,
anashangaa kuona kuwa, imekuwa ni desturi kubwa kwa wasanii wengi hapa nchini,
hususan chipukizi wanapotoka kundi moja kwenda jingine, kuanzisha chuki kati
yao na kundi walilohama.
"Binafsi,
naona jitihada ndio silaha nzuri zaidi kwa msanii, kwasababu hata mimi
nilipotoka Jahazi Modern sikuanza malumbano, ingawa wakati mwingine tulikuwa
tukikosana kama ilivyo kwa wengine wote kwenye sekta mbalimbali," anasema
Isha.
Anasema
kuwa, jambo analopaswa kulizingatia msanii ni jinsi atakavyoweza kusimama
jukwaani kuimba na kumudu kuwanyanyua vitini japo mashabiki watano, na si
kutafuta umaarufu kupitia migongano isiyona msingi.
Kuhusiana
na suala la kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Thabit, Isha anasema kuwa
alishakataa mara nyingi na ataendelea kukataa siku zote, huku akiweka wazi kuwa
uhusiano wake na Thabit unaishia kwenye muziki pekee.
Anaeleza
kuwa, Thabit, kati ya wapapasa vinanda mahiri hapa nchini, ni Mkurugenzi
mwenzie ndani ya Mashauzi Classic, ambako pia anamuheshimu akimwita ‘mjomba’
kutokana na kuwa ni mkubwa zaidi kwake, aliyeanza muziki kabla yake.
“Kiukweli,
mtu ukishakuwa maarufu kuna mambo ambayo huwezi kuyaepuka, hivyo kwa upande
wangu, nazipokea kashfa na shutuma zote ninazorushiwa na kuzichukulia kuwa ni
kati ya changamoto muhimu katika maisha ya ustaa,” anasema Isha.
Hata
hivyo, Isha anasema kuwa, yote yanayosemwa kwa nia mbaya kwake, yanampa ari,
kasi pamoja na nguvu ya kujituma na kujibidiisha zaidi jukwaani ili kuhakikisha
kuwa, malengo ya wasiopenda maendeleo yake hayatimii kirahisi.
Kufuatia
hali hiyo sasa hivi ni muimbaji wa kundi la Kings modern taarabu ambapo kwa
sasa ameshandaanymbo inayotambulika ‘Kash kash za mapenzi’itakayoanza kusikika
mwisho wa mwezi huu.
Anasema
kutokana na kujua umuhimu w kazi yake amewahidi wshabiki wa muziki wa taarabu
kuendelea kuwapa burudani kama kawaida yake.
MWISHO