Thursday, January 5, 2012

Waliokumbwana mafuriko dar wapingiwa debe na wabunge Dar

Mwandishi wetu

MBUNGE wa jimbo la Kigamboni Faustine Ndugulile ameitaka serikali kutowapeleka katik aviwanja walivyovitenga wakati waliokubwa na mafuriko waliopo katika kambi ya shule ya msingi Kiburugwa Mbagala Wilaya ya Temeke.

Akizungumza na blogs hii mbunge huyo alisema atakutana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu kuzungumzia sula la wananchi hao kutohamishwa katika maeneo hayo yaliyotengwa na serikali.

"Nitakutana na mkuu wa mkoa wa DSM na kjadiliana kuweza kutafuta viwanja vilivyopo Mbgala na kuwapatia watu hao kuliko kuhamisha njwe ya hapo kutokana na hali yao kimaisha waliyoizoea,"alisema Dk Ndugulile

Ndugulile alisema wananchi hao watakuwa na wakati mgumu kama serikali itawahamisha kutoka mbagala na kuhamia katika makazi hayo mapya huku wakiwa wameshazoea makazi yao ya kila siku walioyazoea ukilinganisha na shughuli zao za kila siku katika mji wa mbagala.